Uchaguzi wa kura za maoni za kuwatafuta wagombea ubunge na udiwani katika majimbo mawili ya Tarime mkoani Mara umehairishwa baada ya kukamatwa kwa karatasi maalum za kupigiwa kura zikiwa tayari zimepigwa kwa majina yawagombea wawili katika majimbo hayo.
Akizungumza muda mfupi baada ya karatasi hizo kukamatwa,mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Tarime Bw.Rashid Bugomba,amesema zaidi ya karatasi elfu 20 zimekamatwa zikiwa na majina ya mh gaudencia kabaka wa jimbo la Tarime mjini na Mh. Nyambari Nyangwine jimbo la Tarime vijijini na kwamba wakati tatizo hilo likitatuli ikiwa ni pamoja na kutafuta karatasi nyingine za kupigia kura lazima uchaguzi huo sasa usimamishwe kutokana na dosari hizo.
Baadhi ya wagombea katika majimbo hayo wamesema kuwa ukiukwaji huo mkubwa wa uchaguzi ndani ya CCM umefanywa na watu wenye fedha unaweza kuharibu kabisa zoezi zima la uchaguzi huo hata kama uchaguzi huo utahairishwa endapo wagombea hao watarusiwa kuendelea na zoezi hilo.
Nao baadhi ya wapiga kura wa katika uchaguzi huo wa kura za maoni ndani ya CCM Wilayani Tarime wamedai hujuma hiyo ni kubwa imetengenezwa na baadhi ya watendaji wa CCM ngazi ya wilaya.
Hata hivyo wagombea ambao picha zao zinaonekana katika karatasi hizo zikiwa tayari zimepgwa Mh.Gaudencia Kabaka na Mh.Nyambari Nyangwine wote kwa pamoja walipotafutwa kwa njia ya simu kwa nyakati tofauti hawakupatikana kuzungumzia sakata hilo baada ya simu zao kuita kisha kizimwa na kwamba juhudi za kuwatafuta bado zinaendelea.
