Polisi waua kwa risasi mkoani Morogoro

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limemuua mtu anayedaiwa kuwa jambazi katika majibizano ya risasi katika tukio la utekaji na uporaji lililotokea eneo la Chemchem kijiji cha Nakafuru tarafa ya Lupilo Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro.
 
Hata hivyo, majambazi wengine waliohusika katika tukio hilo, walifanikiwa kukimbia baada ya kufanya uporaji huo.
 
 Aliyeuawa ametambulika kwa kutumia kitambulisho alichokutwa nacho chenye jina la Elias Masongo, mkazi wa jijini Dar es Salaam.
 
 Aidha, majambazi hayo pia yalimuua Hassan Matundu (28), mkazi wa Michenga, Ifakara aliyekuwa akisafiri na mama yake, Damiana Sam, kwa kutumia usafiri wa pikipiki kisha kumpora Sh. 200,000 na simu ya mkononi.

 Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Leonard Paul,  alisema tukio hilo lilitokea Agosti 24, mwaka huu saa 2:00 usiku.
 
‘’Tulipata taarifa muda mfupi baada ya kutokea kwa tukio hilo na polisi walipofika eneo hilo, walikuta majambazi hayo yakiendelea kufanya uporaji,” alisema.
 
 Kamanda Paul alisema polisi walianza kuwarushia risasi majambazi hao na kumuua mmoja na wengine walifanikiwa kukimbia.
 
Alisema wakati wakiendelea na uporaji huo, majambazi hayo yalifunga barabara kwa kuweka mawe makubwa na magogo ya miti.
 
Kamanda Paul alisema polisi wanaendelea kuwasaka majambazi mengine yalikimbia.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo