Mbaroni kwa tuhuma za kukutwa na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)

Mkazi wa Kayenzi Manispaa ya Morogoro, Rahim Laswai (30), ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kukutwa na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akiwa amezivaa na cheo cha Koplo.
 
 Mtuhumiwa huyo alikamatwa Agosti 21, mwaka huu saa 9:00 alasiri eneo la Mafiga, Manispaa ya Morogoro.
 
 Kamanda Leonard Paulo alisema mtuhumiwa huyo alitiwa mbaroni wakati akisubiri usafiri kwenda jijini Dar es Salaam na alipohojiwa ilibainika kuwa jina lake halisi ni Abdallah Kassim, mkazi wa tarafa ya Mngeta, Ifakara wilayani Kilombero.
 
 Aidha, Kamanda huyo alisema kuwa mtuhumiwa huyo alipopekuliwa katika chumba chake alichokuwa akiishi kilichopo eneo la Kayenzi, zilikutwa kofia tatu za JWTZ, muhuri wa JKT Oljoro na kwamba shati na kofia zilikuwa zikifanana na sare za jeshi la Marekani na picha alizokuwa amepiga akiwa na sare hizo.
 
 Alisema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili baada ya upelelezi wa Jeshi Polisi  kukamilika.  


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo