Mpya hii kuhusu mauaji ya Albino kuwagusa watu hawa.....

WATANZANIA  waishio Marekani wameguswa na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), yanayotokea nchini Tanzania na kuamua kujitoa katika kupinga mauaji ya hayo.

Hayo yameelezwa na Mwakilishi wa Diaspora hao Honeymoon Aljabri wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam
Amesema kuwa kukithiri kwa mauji ya albino kumewafanya washindwe kuvumilia na kuuamua kuja nyumbani Tanzania ili kuhamasisha kupinga kupitia vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya kijamii kwa kutoa elimu kwa jamii ya kuwalinda na kutoa ushikiano na vyombo mbalimbali vya usalama
Aljabri amesema kuwa wataanza kufanya uhamasishaji huu kwenye mkoa wa Geita kutokana na kuwa kanda hiyo imekuwa miongoni mwa sehemu zilizokithiri mauaji hayo
“ kaulimbiu ya kampeni hiyo ‘je ningekuwa mimi albino ungenihukumu kifo’ (It could be me albino) na sisi tuanajisikia vibaya sana tukiwa ughaibuni tunapoambiwa kinachoendelea nchi kwetu,” amesema.
Ameongeza kwa kuzitaka taasisi nyingine kuwaunga mkono katika kampeni hiyo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo