Balaaa: Matokeo ya kura za maoni CCM ngazi ya Ubunge jimbo la Makete yafutwa

Matokeo ya kura za maoni ngazi ya Ubunge Jimbo la Makete mkoani Njombe yaliyotangazwa usiku wa Jumapili 02.08.2015 na kumpa ushindi Dkt Binilith Mahenge yamefutwa

Taarifa iliyoifikia eddy blog inasema kwamba matokeo hayo yamekosewa na hivyo kufutwa na yatatangazwa upya baada ya kuyahesabu upya

hali hiyo imepelekea wananchi kufurika na kupiga kambi katika ofisi za CCM makao makuu ya wilaya ya Makete kusubiria kwa hamu huku wengine wakidhani huenda ukafanyika uchakachuaji

Akiongea na mtandao huu kwa njia ya simu kaimu katibu wa CCM wilaya ya Makete ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi huo wa CCM Bw. Salum Choni amekiri kuwepo kwa wananchi wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa wagombea hao kuzingira ofisi za chama kushinikiza matokeo hayo yatoke

Hadi tunaondoka eneo la tukio majira ya saa mbili usiku jana matokeo bado hayajatangazwa


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo