Vituko Iringa: Wagombea wagomea kura zilizopigwa saa 12 asubuhi


KUTOKA Kilolo, upigaji wa kura za maoni katika jimbo hilo ulitaka kuingia dosari baada ya kuwepo kwa taarifa ya baadhi ya vituo kufunguliwa saa 12 asubuhi badala ya saa mbili.

Baadhi ya wananchi waliowahi katika vituo hivyo walipiga kura; kura zilizolalamikiwa na baadhi ya wagombea kwa madai kwamba zilipigwa mapema ili kumnufaisha mmoja kati ya wagombea waliotia nia katika jimbo hilo.

Katibu wa Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga alimaliza sintofahamu hiyo kwa kukubaliana na wagombea wote, kura zilizopigwa zihesabiwe ili kuthibitisha madai hayo.

Baada ya kufungua masanduku hayo ya kupigia kura mbele ya mawakala wa wagombea wote ilionekana kuwa wale waliokuwa wakilalamika kuibiwa  kura ndio walionekana kuwa na kura nyingi kuliko waliyekuwa wakimlalamikia.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo