Mwigizaji wa filamu za vichekesho wa Kenya Benson Wanjau maarufu kama Mzee Ojwang (pichani) amefariki dunia Jumapili jioni katika hospitali ya Taifa ya Kenyatta National alikokuwa amelazwa kwa matibabu. Taarifa kutoka NAirobi zinasema alikuwa anaumwa "Nimonia" (Pneumonia).
Marehemu Mzee Ojwang alijipatia umaarufu mkubwa Afrika Mashariki kwa vituko vyake kwenye filamu za Vitimbi, Vioja Mahakami, Vituko na Kinyonga. Alikuwa haonekani kwa muda mrefu kwenye televisheni za Kenya na mashabiki wake wakiwemo wa Tanzania walikuwa hawaishi kumuulizia aliko bila kupata jibu.
Mola aiweke Mahali pema roho
ya Mzee Ojwang - Amin.
Chanzo na habari kamili BOFYA HAPA BREAKING: Comedian Mzee Ojwang of the famed Vitimbi program has passed on. #RIPMzeeOjwang pic.twitter.com/jPZFQBHDAM
— Horizon Post News (@Horizon_Post) July 12, 2015
RIP Mzee Ojwang..doh https://t.co/mot1WWnA99
— ChoirMaster... (@MwanaFA) July 12, 2015
R.I.P Mzee Ojwang tutakumiss sana #theGOAT https://t.co/kf1bjC9DHL
— Jua Cali (@juacaliGenge) July 12, 2015
Veteran TV comedian Benson Wanjau aka Mzee Ojwang' passes on while undergoing treatment at Kenyatta National Hospital
— Citizen TV Kenya (@citizentvkenya) July 12, 2015