BREAKING NEWS: WATU KADHAA WAUWAWA, SILAHA ZAPORWA BAADA YA MAJAMBAZI KUVAMIA KITUO KIDOGO CHA POLISI CHA SITAKISHARI, UKONGA

Habari zilizotufikia chumba cha habari  zinasema kwamba watu kadhaa wameuwawa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, baada ya kuvamia kituo kidogo cha Polisi cha Sitakishari, Ukonga jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo.

Habari ambazo hazijathibitishwa zinasema kwamba askari polisi kadhaa kituoni hapo pamoja na raia mmoja wameuwawa. Silaha kadhaa pia inasemekana zimeporwa na askari wako eneo la tukio hivi sasa.

Tunaendelea kufuatilia taarifa hii na tutawajuza maendeleo yake kadri tutapopata fununu zaidi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo