Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamelaani vitendo
vya kifisadi vinavyoendelea kwenye baadhi ya taasisi za Wizara ya
Nishati na Madini na kulitaka bunge kuunda Kamati teule ya kuchunguza wa
ufisadi wa Shilingi bilioni 200 kwenye akaunti inayojulikana kwa jina
la Escrow fedha ambazo zinadaiwa kupotea kwenye mazingira ya
kutatanisha.
akaunti hiyo ilifunguliwa kufuatia mgogoro baina ya Kampuni ya kufua umeme ya IPTL na
Tanesco ambapo Shirika hilo la Umeme nchini lilipaswa kuilipa Kampuni
ya IPTL kupitia akaunti hiyo hadi hapo mgogoro huo utakapomalizika
ambapo fedha hizo zinadaiwa kupotea kinyemela.
Kwa upande wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini inasema
kuna haja ya fedha za miradi kutolewa kwa wakati ili kusaidia
upatikanaji wa uhakika wa nishati ya umeme nchini.
Awali
akiwasilisha bajeti hiyo Waziri mwenye dhamana Profesa Sospeter Muhongo
anasema bado kuna fikra potofu kuwa serikali haijawawezesha watanzania
kuwekeza kwenye sekta ya madini.
Wizara ya Nishati na Madini
imeomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi Trioni 1, bilioni 82 katika
mwaka mpya wa fedha 2014/2015 ambapo miongoni mwa fedha hizo Shilingi
Bilioni 957.1 sawa na asilimia 88.4 ya bajeti hiyo kutumika kwenye
miradi ya maendeleo huku Shilingi Bilioni 125.3 sawa na asilimia 11.6
kwajili ya matumizi ya kawaida