Kundi la waendesha pikipiki maarufu kama boda boda kutoka vituo vya kawe,bondeni hadi Tangibovu wamelalamikia na kupinga kukithiri kwa uonevu wa makundi yanayojiita ulinzi shirikishi,polisi jamii na Tambaza dhidi yao wakidai kuwatoza fedha nyingi mara kwa mara kama adhabu za usalama barabarani ya kati ya shilingi elfu hamsini hadi laki moja bila ya stakabadhi.
Katika malalamiko hayo walieleza wazi kutokuwa na ugomvi na askari polisi wa usalama barabarani zaidi ya makundi hayo ambayo hayana sare wala vitambulisho ambao kuwakuta katika makutano ya barabara na kuwanyang”anya funguo kwa maelezo ya kutoa fedha hizo kabla ya kupelekwa kwenye vituo vya polisi na wakati mwingine huwafanya kusababisha ajali kwa hofu ya kuwakimbia.
Katika tamko lao lilitolewa na mwenyekiti wao Bw. Kalos Mbwalo wanamuomba mkuu wa kikosi cha usalama barabarani nchini pamoja na serikali kutambua sekta hiyo kuwa ni ajira kama ajira zingine na kutazama upya ushiriki wa makundi hayo katika shughuli za usalama barabarani kutokana na kuonekana kujitwisha majukumu ya polisi huku wakiwa hawana weledi wa kutosha na kujikuta wakigeuza shughuli hizo kuwa miradi ya kujinufaisha na hofu ya vikundi hivyo kuwa nyuma ya baadhi ya viongozi.
mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa kiondondoni kamanda Awadhi Haji Akiongea kwa njia ya simu ambaye pamoja na kueleza mbinu za kikosi chake kufanyakzi kwa kutumia askari waliovaa kiraia amesema kwa malalamiko hayo ipo haja ya madereva hao kufika ofisi kwao kutoa ushirikiano ili waweze kubaini watu hao wanaolipaka matope jeshi la polisi na kuwachukulia hatua za kisheria.