Polisi jijini Dar wamewakamata watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wakiwa katika jaribio la kuiba pesa katika benki ya NMB iliyopo Sinza-Mori, Dar.
Tukio hilo limetokea mchana wa JANA katika Benki ya NMB tawi la Sinza-Mori jijini Dar ambapo majambazi hao walikamatwa wakiwa katika harakati za kutekeleza tukio hilo.
Majambazi hao baada ya kukamatwa wamepelekwa katika kituo cha Polisi Mabatini kilichopo Kijitonyama jijini Dar.