Tume ya taifa ya uchaguzi imepeleka vifaa vya uandikishaji daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo wa elektronia BVR katika wilaya zilizopo mipakani huku serikali ya wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera ikiahidi kudhibiti wahamiaji haramu wasijiandikishe kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili kupungguza mwingiliano wa watu.
Eddy blog imeshuhudia vifaa hivyo vikiteremshwa katika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Kyerwa huku semina zikiendelea kwa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kituo ambapo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Bw.George Mkindo akipokea vifaa hivyo amesema kuwa serikali imejipanga kudhibiti wahamiaji haramu kujiandikisha kwenye daftari la kudum la wapiga.
Kwa upandewake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyerwa Bw.Kashunju Runyogote amesema kuwa halmashauri imejipanga kikamilifu kuelimisha jamii ijitokeze kwa wingi kujiandikisha ambapo wananchi 172000 wanatarajiwa kusajiliwa katika daftari la kudumu la wapiga kura wilayani Kyerwa.