"MAHARAMIA" WAKAMATWA MKOANI MARA, WAPORA INJINI 46 ZA BOTI

Jeshi la Polisi mkoa wa Mara limefanikiwa kuwakamata watu  saba wakituhumiwa kufanya vitendo vya uharamia katika ziwa Victoria na kupora injini 46 za boti zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 150 zilizokuwa zikitumiwa na wavuvi kwa ajili ya kuvua samaki ndani ya ziwa hilo katika maeneo ya Kibuyi wilayani Rorya, Etaro wiya ya Butiama na manispaa ya Musoma mkoani humo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mara kamishina msaidizi wa jeshi la polisi Acp Philip Alex Kalangi, amesema watu hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti kufuatia oparesheni kali inayofanywa na  kikosi maalum  cha jeshi la polisi katika maeneo ya nchi kavu na ndani ya ziwa hilo.
 
Aidha kamanda Kalangi, amesema katika  mwendelezo wa oparesheni hiyo, kikosi hicho maalum cha jeshi la polisi kimefanikiwa kukamata Bangi, Pombe haramu ya Gongo pamoja na bunduki moja ya kivita aina ya AK 47 na risasi 20 zinatumika  kwa bunduki aina SAR na SMG.
 
Katika kipindi hicho cha wiki mmoja, pia jeshi hilo la polisi  mkoa wa Mara, kupitia kikosi cha usalama barabarani, limefanikiwa kukamata makosa 181 ya uvunjifu wa sheria za usalama barabarani  ambapo 161 kati ya hayo yametozwa faini ya zaidi  ya shilingi milioni tano


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo