MAKUBWA TENA YAIBUKA KUHUSU HELKOPTA YA MBUNGE PHILEMON NDESAMBURO

Helkopta ya Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, imeleta kizaazaa, baada ya Kada wa CCM, Buni Ramolle ambaye aliikodi kwa ajili ya mikutano yake ya kutangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo hilo, kudai kuwa ni mbovu na ilitaka kumuua.
Kada huyo akaenda mbali na kueleza kuwa kutokana na hitilafu hiyo, ameitaka kampuni ya General Aviation Services (T) Ltd, iliyomkodishia helkopta hiyo, kumrejeshea fedha zake zote alizoilipa kwa ajili ya kuitumia wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Hata hivyo, Ndesamburo ambaye ni mmiliki wa helkopta hiyo kupitia kampuni yake ya Keys Aviation, alikanusha madai hayo akisema kuwa hayana msingi.
“Anasema helikopta ni mbovu wakati ilimpeleka na kumrudisha? Alihoji Ndesamburo na kusisitiza kuwa “tutawaomba wakaguzi wa ndege waifanyie ukaguzi na ripoti hiyo ndio tutaitumia kumshitaki nayo.”
Kuhusu madai ya Ramolle kuwa amerejeshewa fedha zake alizolipa, Ndesamburo alihoji“Tunamrudishia fedha gani wakati hakulipa? Kuwa na Proforma Invoice ndio kulipia?
Awali taarifa zilieleza kuwa Ramolle alitoa tuhuma hizo, baada ya viongozi wa CCM, kumbana wakimtaka aeleze kwa nini ameamua kutumia helkopta ya Ndesamburo ambaye ni mpinzani wake kisiasa.
Lakini tayari Ndesamburo mwenyewe ameshajitokeza hadharani na kudai kuwa helkopta hiyo ni mali yake na kwamba ameingia mkataba wa kuikodisha kwa kampuni ya General Aviation Services (T) Ltd.
Kwa mujibu wa Ramolle, kinachofanyika sasa ni mbinu za kumchafua ndani ya chama ili asiaminike na aenguliwe kama alivyoenguliwa mwaka 2010.
Ramolle alisema kutokana na Ndesamburo kudai helkopta hiyo ni yake, tayari kampuni ya General Aviation Services wamemrudishia fedha zake alizokuwa amekodishia na ameishtaki kampuni hiyo kwa Meneja wa TRA mkoa wa Kilimanjaro kutokana na kutompa risiti ya malipo aliyoyafanya.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo