Waziri wa Magufuli afunguliwa Kesi Mahakama Kuu

Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara leo imetoa zuio la muda( temporary injuction) linalozuia matumizi ya Kanuni za Maudhui ya Kimtandao (Online Content Regulation) ambazo matumizi yake yalipaswa kuanza rasmi Mei 5, 2018

Mahakama imetoa zuio hilo baada ya taasisi sita kuwasilisha mahakamani maombi ya kuzia matumizi ya Kanuni hizo April 30, mwaka huu.
Taasisi zilizowasilisha maombi hayo mahakamani ni Legal and Human Rights Cente (LHRC), Tanzania Human Rights Defenders (THRD), Media Council of Tanzania (MCT), Jamii Media, Tanzania Media Women’s Association (TAMWA) na Tanzania Editors Forum (TEF).
Taasisi hizo katika kesi ya msingi ya mapatio ya kanuni hizo (judicial review) zimewashitaki Waziri wa Habari, Tanzania Communication Authority (TCRA) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Katika maombi ya msingi taasisi hizo zinaiomba Mahakama Kuu kufanya mapitio ya kanuni hizo kwa kigezo kwamba:-
i) Waziri ametumia nguvu ya kisheria nje ya mamlaka yake ( Ultra vires)
ii) Zinakiuka kanuni za usawa (natural justice)
iii) Kanuni hizo zinapingana na haki ya kujieleza ( Freedom of exepression) haki ya kusikilizwa( rights to be heard) , na haki ya usiri ( Privacy rights). Kesi ya msingi imepangwa kusikilizwa tarehe 10 may 2018.
Angalia hapa Chini:>>>>>>>


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo