KIGANJA CHA MTOTO ALBINO CHAKUTWA HUKO MBOZI MKOANI MBEYA

Kiganja cha mtoto Baraka Cosmas mwenye ulemavu wa ngozi kilichokatwa Machi 8 kwenye kijiji cha Kipeta Sumbawanga kimepatikana mwishoni mwa wiki Wilayani Mbozi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi alisema  kiganja hicho kilipatikana kutoka kwa mkazi wa kijiji cha Malonje Sajenti Kalinga ambaye anafanya kazi ya Useremala.
Alisema awali walimkamata mganga mganga wa kupiga ramli ambaye ndiye aliyehusika kukata kiganja hicho na baada ya kumbana Mganga huyo alimtaja Kalinga ndiye aliyemtuma kuleta kiganja hicho cha albino.
“Tulimbana mtuhumiwa akatuambia aliyemtuma ni Kalinga kwa dau la milioni 100″Msangi.
“Polisi walifika kwa mtuhumiwa Kalinga na walipomuhoji kwa kina alikitoa kiganja hicho na kuwakabidhi”
Hadi juzi watu sita walishikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo wakiwemo waliokamatwa mwaka jana na wengine mwaka huu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo