Wakati taifa likielekea kuipigia kura katiba inayopendekezwa kumejitokeza changamoto ya upatikanaji wa katiba hiyo kutokana na kuwepo na machapisho machache ya katiba inayopendekezwa na hivyo kituo cha sheria na haki za binadamu(LHRC) kimeitaka serikali kuchapisha machapisho ya kutosha ya katiba hiyo ili wananchi waweze kuisoma na kuielewa.
Hayo yameelezwa na mwanasheria wa kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) Bi.Geline Fuko wakati akizungumza katika mikutano mbalimbali ya kutoa elimu kuhusiana na katiba inayopendekezwa mjini songea.
Bi.Geline Fuko amesema katika maeneo mbalimbali waliyozunguka wamebaini kuwa machapisho ya katiba pendekezwa yako machache hivyo wameitaka serikali kuchapisha machapisho hayo ya kutosha.
Katika mkutano uliofanyika chuo cha ualimu Songea TTC na kuwashirikisha wanachuo na walimu katika chuo hicho wanachuo wamekosoa katiba pendekezwa kutokidhi matakwa ya wananchi.