Kamanda wa polisi wa mkoa wa ruvuma ACP MIHAYO MSIKHELA amewataja watuhumiwa wa tukio hilo kuwa ni Boniface Simwanza mwenye miaka 41 raia wa zambia,Adamu Msongore mwenye miaka 26 mkazi wa tunduma mkoani mbeya na Hatman Steven mkazi wa makumbusho Songea huku pia wakiwa na malighafi za kutengeneza dola bandia.
Kamanda Msikhela amesema kuwa polisi inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na utakapokamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za tukio hilo.
Kufuatia tukio hilo jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma linawataka wananchi hasa wafanyabiashara kuwa waangalifu na matapeli wanaotengeneza noti bandia