AJALI HII MBAYA YA GARI YASABABISHA TENA MAUAJI

Kano-Collapse
Hii picha ya ajali nimeiona kwenye baadhi ya mitandao ya Nigeria, imenishtua nikaona niifatilie ajali imetokeaje.
Ajali imetokea Kano, Nigeria.. watu saba wamefariki, Polisi wanafanya uchunguzi wa tukio hili.. ajali hiyo imetokana na kuanguka kwa daraja la waenda kwa miguu lilil0kuwa likiendelea kujengwa katika barabara.
Mafundi waliokuwa wanajenga waliwakataza watu wasipite na magari chini ya daraja kwa sababu bado kazi ya ujenzi ilikuwa ikiendelea, huyo dereva wa taxi alikiuka agizo hilo.. alikuwa anakatisha na gari ikiwa na abiria, daraja likaanguka.. wamefariki watu saba..“– Magaji Majiya, msemaji wa Jeshi la Polisi.
d3
Daraja ambalo lilikuwa likijengwa lilikuwa kama hili.
Mara nyingi ujenzi ukiwa unaendelea kwenye barabara kunakuwa na vibao vya maelekezo lakini watu wengi huwa hawazingatii maelekezo, ndicho ambacho kimetokea kwenye hii ajali ya Nigeria.
Picha nyingine za ajali hiyo hizi hapa..
IMG-20150427-WA0043
IMG-20150427-WA0044
IMG-20150427-WA0045
Hii ajali abiria waliokuwemo kwenye taxi hiyo wala dereva hata hawakujua hiki kingetokea, #RIP kwa watu wetu waliofariki.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo