MUME AMUUA MKEWE KINYAMA SIKU NNE BAADA YA KUMUOA KWA HARUSI

Handcuffed PrisonerWivu wa mapenzi upo, lakini huyu jamaa aliamua kufanya ukatili kwa mpenzi wake, ilikuwa siku nne tu baada ya kufunga ndoa zao.
Hii stori imetoka Brazil baada ya mume kuamua kumuua mke wake kisa tu huangaliwa na wanaume ikiwa ni siku ya nne tu tangu afunge naye ndoa kanisani.
Wawili hao ambao walikuwa wakiishi katika mji wa Rio De Janeiro, kwa sasa mwanaume huyo ameshikiliwa na polisi na kufunguliwa kesi ya mauaji.
Mwanaume huyo Vieira Severiano alimuua mkewe Cixera Alves De Sena ambaye alikuwa ni mcheza shoo katika bustani ya sehemu waliyokuwa wakiishi ambapo camera ziliweza kunasa tukio zima.
Video hiyo ilimwonyesha mwanaume huyo akigombana na mkewe kwa muda kabla ya kumpiga risasi tano usoni iliyosababisha kupoteza maisha yake.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo