ASKARI POLISI AGEUKA KUWA MHUDUMU WA AFYA

3d-abstract_other_soldier-in-sunset_27703
Kutokana na tatizo la hofu ya usalama Kenya leo tulisikia ishu ya walimu kugoma kwenda kufanya kazi maeneo ya kaskazini mwa Kenya.. kingine ilikuwa ishu ya wahudumu wa afya pia kukimbia maeneo hayo kutokana na hofu ya mashambulizi hayo pia.
Kaskazini mwa Kenya hali sio shwari sana, hii story inatoka maeneo ya Turkana ambako Afisa mmoja wa Polisi Alfred Lokori amelazimika kuchukua jukumu la kuwahudumia wenyeji wa eneo hilo katika kituo cha Afya cha Lomelo, kituo hicho hakina wahudumu kabisa.
sasa nimekuwa Askari mahali pengine na mahali pengine nimekuwa ni daktari “; Alfred Lokori.
Tukio kama hili liliripotiwa wiki iliyopita katika kaunti hiyohiyo ya Turkana ambako kijana mmoja alijitokeza kufanya kazi ya udaktari ambayo haifahamu kutokana na ukosefu wa wahudumu wa Afya katika eneo hilokutokana na kukosekana kwa usalama.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo