Wananchi wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura katika zoezi litakaloanza kwa awamu katika kata za wilaya hiyo
Kwa kuanza zoezi hilo litaanza rasmi kesho Jumatatu Machi 16 katika baadhi ya kata na zoezi hilo litaendelea kwa kata zote hadi zimalizike
Akizungumza na mtandao huu kaimu Afisa ucaguzi wilaya ya Makete Bw. Gregory Emmanuel amesema wilaya imejipanga vizuri kuhakikisha zoezi hilo linafanyika ipasavyo kama serikali inavyohitaji hivyo kuwataka wananchi wote kujitokeza kujiandikisha kwa kuwa kila aliyetimiza umri wa miaka 18 na kuendelea ataandikishwa
Maboresho ya daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo mpya wa BVR linaendelea mkoani Njombe ambapo kwa wilaya ya Makete miongoni mwa kata zitakazoanza kesho ni Tandala na Lupalilo