Serikali
imesema haitasita kuwachukulia hatiua za kisheria watendaji wa
vijiji,kata, wilaya na mkoa watakao shindwa kudhibiti mauaji ya walemavu
wa ngozi kwenye maeneo yao na kuwataka wananchi kutowachagua wanasiasa
wanaojihusisha na imani potofu za kishirikina ili kupungumza mauaji ya
kinyama yanayotia doa nchi ya tanzania katika mataifa yanayoendelea
duniani.
Changamoto hiyo imetolewa jijini mwanza katika mkutano wa hadhara
ulioitishwa na kamati ya amani ya viongozi wa dini mkoa wa mwanza kwa
lengo la kulaani mauaji ya walemavu wa ngozi albino yaliyoibuka kwa
staili ya kuteka nyara watoto chini ya umri wa miaka mitano ambapo
mkutano huo umehudhuriwa na maelfu ya wananchi kutoka mikoa ya kanda ya
ziwa, wanasiasa, viongozi wa dini, watendaji wa serikali, wafanyabia shara
wakubwa kwa wadogo,wasomi kutoka vyuo vya elimu ya juu na wasanii
maarufu hapa nchini ambapo waziri mkuu wa Tanzania alialikwa kama mgeni
rasmi na kuwakilishwa na waziri wa nchi uratibu na uhusiano katika ofisi
ya rais Mh.Mary Nagu ambaye amesema kuwa serikali haitavumilia unyama
unaotendeka kwa jamii.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa mwanza Bw.Magesa Mulongo amewataka
wakuu wa wilaya kuwakamata watuhumiwa bila huruma yoyote na kwamba
atakayebainika ameshindwa kutimiza wajibu wake atachukuliwa hatua za
kisheria ikiwa ni pamoja na kuachishwa kazi ili kutekeleza kauli mbiu ya
mkoa wa mwanza juu ya walemavu wa ngozi inayosema tunaishi
pamoja,tunakula pamoja,tunacheza pamoja katika nchi moja
Katika kongamano hilo wananchi kwa pamoja wamejitolea kuchangia
fedha chama cha walemavu wa ngozi mkoa wa mwanza ambapo zaidi ya
shilingi milioni sita zimepatikana huku wananchi wakichangia kiasi cha
shilingi milioni moja,waziri wa nchi uratibu na uhusiano katika ofisi ya
rais Mh.Mary Nagu amechangia kiasi cha shilingi milioni moja na
mfanyabiashara maarufu jijini mwanza Bw.All Taf Dogo Mansoor ametoa
shilingi milioni nne ambapo viongozi wa chama cha walemavu wa ngozi
mkoa wa mwanza wameiomba jamii iwathamini kwa kuwalinda.