Chama
cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA),kimeitaka serikali kuiongezea
tume ya taifa ya uchaguzi (NEC), vifaa vya kutosha na muda ili
kufanikisha zoezi la uandikishaji wa wapigakura kwa mfumo wa BIOMETRIC
VOTERS’ REGISTRATION – BVR, ili kuhakikisha kila mtanzania mwenye sifa
ya kupiga kura anaandikishwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao.
Akifungua mkutano wa kamati tendaji kanda ya ziwa victoria, baraza
la uongozi wa kanda hiyo inayoundwa na mikoa ya kagera, geita na mwanza
pamoja na wadau, mwenyekiti wa chadema taifa Mh. Freeman Mbowe ameitaka
serikali kuipatia tume ya taifa ya uchaguzi fedha za kutosha ili zoezi
linaloendelea la kuandikisha wapigakura kwenye daftari la kudumu liweze
kufanikiwa, ambapo amesema tume hiyo hadi sasa imepokea mashine 80 tu za
BVR kati ya 800 zinazohitajika nchi nzima.
Akizungumzia mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe
yanayoendelea kutokea katika mikoa ya kanda ya ziwa kwa imani za
ushirikina na tamaa ya baadhi ya watu kujipatia utajiri wa haraka
haraka, ambapo hadi sasa inakadiriwa kuwa watu 76 wenye UALBINISM
wamekwisha uawa hapa nchini tangu mauaji hayo yalipoibuka, mwenyekiti
huyo wa chama cha demokrasia na maendeleo amesema jambo hilo linapaswa
kukomeshwa na serikali kwa nguvu zote na watuhumiwa kufikishwa mbele ya
vyombo vya dola.
Akimkaribisha kufungua mkutano huo wa siku mbili, naibu katibu mkuu
wa chadema – Zanzibar Salum Mwalimu amesema ni jambo la kusitikisha
kuona serikali ikijivunia kuzindua kivuko kipya cha MV. DAR ES SALAAM
kitakachosafirisha abiria kati ya Dar es salaam na Bagamoyo na kutumia
saa nne kwa maelezo kwamba kitasaidia kupunguza msongamano na foleni.