Msimamizi
wa mradi wa FAO kijiji cha Kiroka mkoani Morogoro, Ajuaye Sigalla,
akitoa muhtasari wa maendeleo ya mradi FAO unaotekelezwa na wanakikundi
wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI) mbele ya Mratibu Mkazi wa Mashirika
ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez (kushoto) na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini,
Filiberto Sebregondi walipofanya ziara ya kugagua miradi yao ya
maendeleo mkoani Morogoro.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Mwandishi wetu, Morogoro
BALOZI
wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi ametembelea skimu
ya umwagiliaji ya Kiroka na kusema kwamba atahakikisha kwamba kwa
kushirikiana na wadau wengine ikiwamo serikali wataendelea kusaidia
wananchi kujiinua kiuchumi.
Akiwa
katika skimu hiyo inayosaidiwa na Shirika la Chakula duniani (FAO)
ametaka miradi ya maendeleo nchini kutowaacha nyuma wanawake na watoto
kwani wao ndio msingi wa maendeleo ya kijamii kuanzia ngazi ya kaya hadi
Taifa.
Balozi
huyo ambaye anatarajiwa kurejea Ulaya mwaka huu baada ya kumaliza muda
wake wa uwakilishi nchini amesema kwamba kuwapo kwa asilimia 60 ya
wafaidika na mradi huo wa Mpunga kuwa wanawake kumesaidia sana kuamsha
maendeleo ambayo yanatakiwa kuendelea kusimamiwa.
"Wanawake
wamefanikiwa kupeleka watoto wao shuleni. kuwapatia chakula
kinachostahiki na kupata kipato na katika hili ni vyema wasiachwe nyuma
kimaendeleo" alisema balozi huyo.
Balozi
wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi akizungumza na
wanakikundi wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI) wanaofadhiliwa na FAO
wakati wa ziara ya kutembelea miradi inayofadhiliwa na wadau wa
maendeleo ambapo mradi wa Kiroka unafadhiliwa na shirika la Umoja wa
Mataifa la FAO huku mradi wa makazi mapya kwa waathirika wa mafuriko
Kilosa ukifadhiwa na Ubalozi wa Umoja wa Ulaya. Kushoto kwake ni
Msimamizi wa mradi wa FAO kijiji cha Kiroka mkoani Morogoro, Ajuaye
Sigalla.
Alisema
kwamba amefurahishwa sana na mradi huo na kusema kwamba Umoja wake
utaendelea kushirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa na serikali
katika kuhakikisha kwamba mwananchi wa kawaida wa Tanzania anapata
maisha bora.
Mradi
wa Kiroka ambao unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya FAO na benki ya
NMB ikishirikiana na RaboBank umelenga kuboresha kilimo cha Mpunga na
pia kuwawezesha wakulima hao kuwa na nafasi ya kupata fedha za
kuendeleza majukumu yao.
Ili kufanikisha hilo wakulima wanapatiwa elimu ya fedha na pia utunzaji wa nafaka wa pamoja na mikakati ya mauzo.
Balozi
wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi akifafanua jambo
wakati akitoa salamu kwa wanakikundi wa Umoja wa Wakulima Kiroka
(UWAKI). Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji cha Kiroka, Mbaraka
Mnebe, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa
shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na Msimamizi
wa mradi wa FAO kijiji cha Kiroka mkoani Morogoro, Ajuaye Sigalla.
Mradi
huo ulioanza 2004 na kutarajiwa kuisha Juni mwakani unatekelezwa 2018
umelenga kufungua fursa kwa wanawake na wanaume na kuongeza uzalishaji,
kusaka masoko, kupata njia ya kupata mikopo na kujenga uwezo wa
kufanikisha shughuli za maendeleo kwenye skimu.
Mradi huo unatarajiwa kutumia dola za Marekani 737,000 hadi utakapokamilika.
Wakizungumza
na balozi huyo kuelezea mazingira yao wakulima walishukuru msaada
unaotoka katika mashirika ya kimataifa na kuwaomba kusaidia kuwapatia
fursa zaidi za maendeleo kwa elimu wanayoipata.
Wamesema
mabadiliko yaliyosababishwa na elimu yamewafanya wazalishe Mpunga kwa
wingi katika eneo dogo na kufungua fursa za masoko kwa hifadhi na
utafutaji masoko wa pamoja.
Katibu
wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI), Muhidin Kigadu akielezea mafanikio
waliyoyapata tangu walipoanza kupewa mafunzo ya kilimo bora
yanayofadhiliwa na Shirika la FAO mbele ya ugeni huo.
Mradi
huo ambao ulianza na Watu wa Sua kama watoa elimu sasa wanapigwa msasa
na Taasisi ya maendeleo mjini na Vijijini (RUDI) kwa lengo la
kuhakikisha kwamba wanatumia mfumo wa Asia wa ulimaji wa Mpunga kwa
kutumia maji kidogo huku wakihifadhi ghalani kusubiri bei nzuri.
Katika
ziara hiyo ya karibuni ya Balozi huyo akiambatana na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, viongozi hao walipata nafasi ya
kusikiliza changamoto za wakulima katika mradi huo ambapo uzalishaji
sasa umeongezeka kutoka gunia tano kwa eka kufikia gunia 25 kwa kulima
kitaalamu.
Katibu
wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI), Muhidin Kigadu alisema mradi huo
ambao ulianza Februari 21,2012 umewajengea uwezo wakulima wa mlimani
kutengeneza makinga maji huku wakulima wa kwenye skimu wakilima kilimo
cha mashadidi.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Kiroka, Mbaraka Mnebe akielezea jinsi skimu
ilivyowasaidia kuinua maisha ya wananchi kwa kuwapatia elimu
iliyowaletea mafanikio makubwa yaliyowezesha kulima kisasa na
kubadilisha maisha yao hasa katika makazi na huduma za jamii na
kuwapeleka watoto shule.
Alisema wanawashukuru wahisani kwa kuwawezesha kurejesha uoto wa kijani ikiwa na pamoja na kuwa na kilimo cha matunda.
Naye
Mwenyekiti wa kijiji cha Kiroka, Mbaraka Mnebe amesema skimu
imewasaidia kuinua maisha ya wananchi kwa kuwapatia elimu iliyowaletea
mafanikio makubwa yaliyowezesha kulima kisasa na kubadilisha maisha yao
hasa katika makazi na huduma za jamii na kuwapeleka watoto shule.
Aidha wakulima wamefanikiwa kununua vyombo vya usafiri vya moto kama Pikipiki na kuachana na Baiskeli.
Mwanachama
wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI), mkoani Morogoro, Bi. Asha Bogasi
akitoa ushuhuda jinsi maisha yao yalivyobadilika mpaka wanaweza kusaidia
na waume zao kusomesha watoto wao kutokana na skimu ya mradi huo.
Hata
hivyo amesema pamoja mafanikio hayo wanachangamoto hasa ya masoko na
elimu ambayo wanadhani wanaihitaji zaidi huku akisisitiza zaidi kwamba
elimu inatakiwa hata kama wamemaliza mradi na wahisani kuondoka.
Mradi
bado ambao haujakamilika kwani kati ya hekta 147 za mradi ni kama hekta
40 zinazotumuka kwa kuwa miundombinu haijatawanyika vya kutosha katika
hekta zote.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akijibu hoja mbalimbali
zilizotolewa na kuwapa pongezi za kuweza kubadilisha maisha yao kupitia
kilimo cha kisasa kinachofadhiliwa na FAO kwa wanachama wa Umoja wa
Wakulima Kiroka (UWAKI) alipofanya ziara ya kukagua mradi huo kijijini
hapo.
Wanachama
wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI) wakiwa wamekusanyika kwenye shule
ya msingi Kiroka wakati wa ugeni wa Shirika la Umoja wa mataifa na
Ubalozi wa Umoja wa Ulaya ulipowatembelea kukagua miradi yao.
Mratibu
mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na Balozi wa Umoja wa Ulaya
wakiondoka kijijini hapo mara baada ya kukutana na kuzungumza
na Wanachama wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI).