Simba wametoa pongezi kwa
watani wao wa jadi Yanga kutokana na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya FC Platinum
ya Zimbabwe.
Yanga imeshinda kwa
mabao hayo na kujiweka katika
nafasi nzuri katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji
ya Simba, Said Tully amesema kwa niaba ya Rais wa Simba, Evans Aveva
wanaipongeza Yanga.
“Yanga ni wawakilishi wa nchi
katika michuano ya kimataifa. Hakika wanastahili pongezi kutokana na kufanya
vema.
“Inapofikia katika suala la
nchi, si vibaya kuwapongeza. Tukirudi kwenye ligi basi upinzani unaendelea.
“Ndiyo maana leo tulikuwa
uwanjani kushuhudia Yanga wakipambana na walifanya vema kwa kweli,” alisema
Tully.
Yanga imeitandika FC Plutinum
kwa mabao hayo matano katika mechi nzuri ya kuvutia kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.