HOSPITALI YA TMJ DAR ES SALAAM YAPEWA SIKU 7 TU, LA SIVYO ITAKIONA CHA MOTO

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, ametoa siku saba kwa Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam, kuhakikisha inajenga mtaro wa kupitisha maji machafu ili kuondokana na majitaka hayo kuingia kwenye mitaro mipya inayojengwa.
Alisema kama hospitali hiyo itapuuza agizo hilo, ndani ya siku saba, serikali itachukua hatua stahiki ikiwamo ya kuzuia kutoa huduma.
Makonda alitoa kauli hiyo alipotembelea kwenye maeneo ya Mikocheni kukagua miundombinu ya barabara na mitaro inayojengwa ili kudhibiti athari za mvua zinazotarajia kunyesha wakati wowote.
Makonda, alishuhudia mtaro wa majitaka ya hospitali hiyo ukitiririsha uchafu kuelekea kwenye mitaro mipya inayojengwa hali iliyosababisha mitaro hiyo kujaa taka kabla ya kukamilika kwake.
Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Mbaraka Mkwiya, alisema miradi ya ujenzi wa mitaro ya maji taka kwenye bonde la mpunga unagharimu takribani Sh. bilioni sita  na barabara tano za mitaa ya Mikocheni na Msasani ambazo zitagharimu Sh. bilioni 3.3 ambayo yote, inatarajia  kukamilika miezi michache ijayo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo