Na
Christina Mwagala
KUFUATIA
kuwepo kwa baadhi
ya viongozi wengi wa serikali na
dini kujihusisha na biashara ya dawa za
kulevya Serikali imedhamiria kuunda chombo chenye nguvu kwa ajili ya
kupambana
nao.
Akizungumza
katika
maadhimisho ya siku ya kupambana na madawa ya kulevya nchini
yaliyofanyika leo
katika viwanja vya shule ya msingi Tandale jijini Dar es Salaam, Waziri
wa mambo
ya ndani Dk Emanuel Nchimbi, alisema biashara ya dawa za kulevya
isipodhibitiwa
ipasavyo kuna hatari ya nchi kushindwa kuongozwa
Nchimbi
aliyemuwakilsha
waziri mkuu alisema athari za dawa za kulevya zinaathiri sekta zote
pasipo kujali
utashi wa mtu, na kwamba wanaoathirika zaidi ni vijana ambao ni nguvu
kazi ya
Taifa.
Alisema
kuwa tabia yawatu kujihusisha na biashara haramu yadawa zakulevya
inazidi kuota
mizizi hapa nchini kutokana na tamaa ya viongozi kutaka kupata utajiri
wa haraka
bila kujali kuwa inaleta madhara makubwa kwa wanachi.
Aliongeza
kuwa
Serikali
imejipanga kukabiliana na tatizo hili nah ivyo hadai sasa tayari imeanza
kuanzisha mchakato wakuhakikisha kuwa serikali
inapata chombo chenye nguvu kiutendaji
cha kupambana na dawa za kulevya ambacho kitanzishwa hivi karibuni
nakuanza
kazi maramoja.
Nchimbi aliongeza kuwa
tatizo la dawa za kulevya bado lipo
hapa nchini na linazidi kukua kila mwaka na hivyo Serikali
kupitia vyombo vya ulinzi na
usalama vinatakiwa kujikita katika kupambana na biashara hizo
ilikuhakikisha
kuwa tatizo hili linakwisha kabisa.
Nchimbi alisema zao la bangi limezidi kuwa tatizo
zaidi kutokana na
kupatikana kirahisi kutokana kuzao hilo kulimwa kwa wingi katika mikoa
iliyo
athirika ikiwemo Tanga, Mbeya na Iringa.
Nahivyo kuagiza kamati za ulinzi na
usalama za mikoa yote hapa nchini kuhakikisha zinasimamia na kuratibu
udhibiti
wa kilimo hiki na kuwasaidia wananchi ili waweze kushiriki katika kilimo
cha
mawazo mbadala.
Madhara ya dawa za
kulevya yamekuwa yakikusababisha
mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali na hivyo kuleta ugumu wa maisha kwa
wananchi,huku
akilituhumukupoea kwa nguvu kazi yataifa siku hadisiku.
Nchimbi alisema kuwa
watumiaji wadazakulevya wamekuwa nikeroi kubwa
kutokana na vijana wengi kupata Magonjwa mbalimbali yamambukizi yakiwemo
ukimwi
na homa ya ini hali inayopelekea
wengiwao kupoteza maisha.
Aidha aliongeza kuwa nchi
inaweza kuingia vitani kutokana
na biashara haramu ya dawa za kulevya kama ilivyotokea nchini Colombia
na
vurugu za magenge yanayojihusisha na biashara hiyo haramu zinazoendelea
hivi
sasa nchini Mexico na hivyo kama nchi yetu haitakuwa makini kwa
kuwashugulikia viongozi wa kisiasa waliojiingiza kwenye
biashara hizo itajikuta inakuwa kama hizo.
“Nchi inapokuwa kitovu
cha biashara haramu ya dawa za
kulevya inajivunjia hadhi ya kimataifa na wananchi wake hushukiwa kila
wanaposafiri nje ya nchi, hupata tabu sana katika viwanja vya ndege vya
kigeni
pindi wanaposafiri kwa kushukiwa na kupekuliwa sana. kwa wale watanzania
ambao
wanajihusisha na biashara hii nje ya nchi watambue kwamba adhabu kali za
vifo
zita wakabili kama hawata jirekebisha”alisema nchimbi.
Hata hivyo Nchimbi
amekiri kuwepo kwa tatizo lar ushwa katika kudhibiti
watumiaji wa madawa ya kulevya miongoni mwa watendaji wa serikali amabapo
alisema kuwa wapo baadhi ya watendaji ambao si waadilifu katika utendaji
kazi wa
kila siku haliinayo sababisha kurudisha nyuma
jitihada za serikali kupiga vita tatizo hilo.
Kaulimbiu ya mwaka huu ni
tujenge jamii yenye afya bila
Dawa za kulevya,na tutoe maoni yakatiba nakushiriki sensa.