Mwili wa aliyekuwa waziri wa nchi ofisi ya Rais utumishi Marehemu Celina Kombani aliyefariki nchini India ambako alikuwa akipatiwa matibabu umewasili jana katika uwanja wa kimataifa wa mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali.
Marehemu Kombani pia alikuwa ni mgombea ubunge katika jimbo la ulanga mashariki Mkoani Morogoro kupitia Chama cha Mapinduzi CCM.
Viongozi waliofika uwanjani hapo akiwemo Katibu Mkuu Kiongozi balozi Ombeni Sefue, Waziri wa Fedha Saada Mkuya, Katibu Mkuu CCM Abdulrahman Kinana na wengineo wamemzungumzia kwa namna tofauti marehemu Kombani kuwa alikuwa ni mchapa kazi lakini kubwa zaidi CCM imebaki na pengo kubwa katika jimbo hilo ambako walikuwa na matarajio makubwa ya kushinda.
Mkurugenzi wa uchaguzi Ramadhani Kailima amebainisha kuwa hadi sasa majimbo mawili yamepoteza wagombea wa ubunge na kata tano za udiwani hivyo uchaguzi umeahirishwa na kampeni zimesimamishwa kwa waliopo katika majimbo na kata hizo kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ambayo inavitaka vyama vilivyosimamisha wagombea kuteua wagombea wapya ndani ya siku 30 tangu kutokea kwa kifo na kuwasilisha tume ya uchaguzi ambayo itatangaza siku ya kufanyika kwa uchaguzi.
Kwa mujibu wa katibu mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue utaratibu wa ratiba kamili ya shughuli za mazishi unaendelea na pindi utakapokamilika wananchi watatangaziwa.
Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani umewasili jana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam |
Familia ya marehemu, viongozi mbalimbali na wananchi wakisubiri mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani ulipowasili jana jioni Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Aliyeshikwa bega wa tatu kushoto ni Mume wa Marehemu Mzee Kombani.
Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani ukiteremshwa baada ya kuwasili jana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Msafara wa mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani ukipelekwa kwenye ambulance baada ya kuwasili jana jioni Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani ukiteremshwa baada ya kuwasili jana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Msafara wa mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani ukipelekwa kwenye ambulance baada ya kuwasili jana jioni Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Spika wa Bunge Mhe Anne Abdallah na viongozi wengine wakiwa Uwanja wa ndege kupokea mwili wa marehemu Kombani. Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii. |