Rais Kikwete Aongoza Mamia Ya Wananchi Katika Kuuaga Mwili Wa Aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni John Komba

Rais Jakaya Mrisho Kikwete  na mkewe Mama salma Kikwete sambamba na viongozi mbali mbali wa kitaifa wamewaongoza mamia ya waombolezaji kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni John Komba katika Viwanja vya Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Mwili wake umepokelewa kwa heshima huku ukiwa umebebwa na Askari maalumu wa bunge huku ndugu jamaa na marafiki wakiwa katika huzuni ya kuondokewa na mpendwa wao huyo aliyefariki duniani katika hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam hapo juzi.

Katika salamu zake kwaniaba ya kambi Rasmi ya upinzani Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Mh.Joshua Nasari ametoa pole kwa marehemu na taifa na kusema kamba kambi rasmi ya upinzani imeguswa na kifo cha mwanasiasa mwenzao kwani kila mmoja atarejea na huko ndiko kila mmoja atakwenda kwa hivyo yatupasa kutengeneza mazingira mazuri kwa familia kwani hakuna ajuaye siku yake ya mwisho ya kufa.
 
Amesema katika kipindi hiki kigumu nidhahiri kwamba kila mmoja anapaswa kusali na kuomba kwani wao kama kambi rasmi ya upinzani imekuwa nisehemu ya kuweka siasa mbali na hivyo kuungana na taifa na familia katika kipindi hiki kigumu.
 Rais Kikwete (katikati) akiwa na makamu wake Gharib Bilal (kushoto) na Anna Makinda katika viwanja vya Karimjee ili kumuaga marehemu Kapteni John Komba.
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa (wa pili kulia) akiwa na mkewe Anna (wa tatu kulia) wakiwasili viwanja vya Karimjee.
Waziri mkuu aliyejiuzulu,Edward Lowassa (kulia)akisalimiana na Mkapa.
Spika wa Bunge, Anna Mkapa (kushoto) akiwa na Mkapa.
Mbunge wa Kinondoni Idd Azzan (kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba (kulia) akiwa viwanja vya Karimjee.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (kulia)akisalimiana na mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale.
Wake wa marehemu Komba, katikati ni mke mkubwa, Salome, na kulia ni mke mdogo.
Miongoni mwa wanafamilia wa marehemu Komba.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo