
Ni majira ya saa 10:30 jioni, mwili wa marehemu Kepten John Komba
ukawasili katika uwanja wa ndege mjini Songea ukiambatana na familia ya
marehemu, viongozi mbalimbali akiwemo katibu wa bunge, na wabunge wote
wa mkoa wa Ruvuma ambapo mapokezi hayo yameongozwa na mkuu wa mkoa wa
Ruvuma, Said Mwambungu.
Na baadaye mwili wa Kepten John Komba ukapelekwa katika uwanja wa
majimaji mjini Songea, ambapo maelfu ya wakazi wa Songea wakiwa
hawaamini kilichotokea na kushikwa na simanzi kubwa wamejitokeza kuuaga
mwili wake huku foleni ikiashiria wazi kwamba siyo wote watakaofanikiwa
kuuona mwili wa Kepten Komba kwa mara ya mwisho.
Mwili wa marehemu Kepten John Komba unatarajiwa kuzikwa Leo
kijijini kwake lituhi wilaya ya nyasa ambapo mazishi yake yataongozwa na
rais Mh. Jakaya Kikwete.