Watu 3 wamefikishwa mahakama ya wilaya ya Chato kusomewa shitaka la mauaji ya mtoto albino Yohana Bahati.

Watu watatu wamefikishwa mahakama ya wilaya ya Chato kusomewa shitaka la mauaji ya mtoto Yohana Bahati aliyeibiwa hatimaye kuuwawa tarehe 15 Februali katika kitongoji cha mapinduzi wilayani Chato mkoani Geita.

Akizungumza na waandishi wa habari, kamanda wa polisi mkoa wa Geita Sacp Joseph konyo amesema watu wengine wawili bado wanahojiwa na jeshi la polisi ili kupata ushahidi unaojitosheleza katika kesi hiyo, amewataja watu waliofikishwa mahakamani ni Bahati Misalaba ambaye ni baba wa Yohana, Juma Lupembe Kilebelo, Manyanda Mandege almaarufu Makongoro mkazi wa wilaya ya Mbogwe na mchimbaji wa dhahabu.
 
Kamanda konyo amesema jeshi la polisi linaendelea na juhudi za kuwakamata wauwaji wa kukodiwa wanaofanya mauaji hayo kwa ujira mdogo wa laki moja ili kudhibiti vitendo vya mauaji katika maeneo ya kanda ya ziwa.
 
Katika tukio jingine jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu watatu wanaosadikika kuwa ni majambazi wazoefu wa kuteka magari barabarani na kuvamia maduka ya fedha mkoani Geita, watu hao Niosca John Bosco, Kapuru Msigwa ustaadhi, na Elias Shigilimelo Bambala.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo