Siku chache kupita baada ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mabere Marando kufichua njama za Mlinzi wa Katibu Mkuu wa Chama hicho Wilbroad Slaa, bwana Khalid Kangezi kupanga mipango ya kumuua katibu huyo huku akishirikiana na Vigogo wa Chama Mapinduzi CCM pamoja na Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa wa Kinondoni,naye Mlinzi huyo ameibuka na kufichua siri nzito ndani ya Chama hicho kikuu cha upinzani nchini..
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kangezi amesema siku ya kifo cha
marehemu Kapteni John Komba alikuwa akitokea nyumbani kwake Mwenge
akielekea kazini nyumbani kwa Dk. Slaa ambapo baada ya kufika getini
aliambiwa na mlinzi wa geti hilo kuwa haruhusiwi kuingia ndani na
alipouliza sababu alijibiwa kuwa taarifa imetoka kwa mke wa Dk. Slaa.
Alipoendelea kuhoji alipewa majibu kwamba
hapaswi kuendelea kumuuliza maswali ndipo aliamua kurudi tena nyumbani
kujipanga kwa siku ambayo ingefuatia huku akiendelea kufanya juhudi za
kumpata Dr. Slaa ili aweze kumuuliza sababu kuu ya kuzuiwa kuingia
ndani.
Siku iliyofuatia ambayo ilikuwa Jumatatu
ambapo Komba alikuwa anatakiwa kuagwa rasmi, alidamka asubuhi na mapema
kuelekea nyumbani kwa Dk. Slaa kwani alijua kuwa naye angetakiwa
kuungana na viongozi wengine kuuaga mwili wa marehemu.
Kwa bahati nzuri alifanikiwa kumkuta nyumbani japokuwa alizuiwa tena kuingia ndani ila majibu aliyopewa na Slaa ni kuwa aongee na mkewe wamalizane mgogoro wao na yeye akasema hakutaka kuingilia mgogoro huo.
Kwa bahati nzuri alifanikiwa kumkuta nyumbani japokuwa alizuiwa tena kuingia ndani ila majibu aliyopewa na Slaa ni kuwa aongee na mkewe wamalizane mgogoro wao na yeye akasema hakutaka kuingilia mgogoro huo.
Kangezi aliongeza kuwa hakutarajia kama
mke wa Slaa angekuwa na mgogoro naye kwani walikuwa wakiitana mtu na
kaka yake kwa vile wanatoka Mkoa wa Kagera.
Kangezi aliendelea kuelezea kuwa hakuamini
kama kweli angeweza kufungiwa nje ya geti la nyumba kutokana na jinsi
alivyokuwa akihangaika katika kuhakikisha ulinzi wa Dk. Slaa kwa nguvu
ya hali ya juu kutokana na masuala ya vyama na ameishi naye kwa muda wa
zaidi ya miaka 14 bila shida wala tuhuma yoyote.
Baada ya kukosa maelewano nyumbani kwa Dk.
Slaa, aliamua kwenda katika ofisi za chama hicho zilizoko Kinondoni kwa
ajili ya kuonana na kiongozi wake ambapo baada ya kufika alidai
alizuiwa na viongozi wa chama hicho tena wakimtaka kuingia katika chumba
maalumu kwa ajili ya kuchukua mahojiano naye ambapo alifanya kama
alivyotakiwa.
Aliwataja viongozi wa chama hicho
aliowakuta humo ambao tayari walimwamuru kuvua nguo zake zote na kubakia
kama alivyozaliwa huku akitishiwa kuuawa.
Humo alitakiwa kueleza mahusianao yake na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Philip Mangula, na watu wa usalama wa taifa ambapo alisema alisulubiwa kwa muda wa saa sita na akatakiwa kuandika katika karatasi kukiri kuwa kweli anawasiliana nao na kutokana na kipigo alichokuwa akikipata, akihofia kuuawa, aliamua kutii matakwa yao.
Humo alitakiwa kueleza mahusianao yake na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Philip Mangula, na watu wa usalama wa taifa ambapo alisema alisulubiwa kwa muda wa saa sita na akatakiwa kuandika katika karatasi kukiri kuwa kweli anawasiliana nao na kutokana na kipigo alichokuwa akikipata, akihofia kuuawa, aliamua kutii matakwa yao.
Siku hiyohiyo majira ya usiku alipelekwa
katika hoteli iliyoko maeneo ya Sinza–Madukani ambapo alipakizwa katika
gari alilokuwemo mwanasheria wa chama chicho, Mabere Malando, hadi
kwenye hoteli waliyokuwa wamechukua vyumba na kumwingiza ndani ambako
walianza tena kumsulubu hadi akaishiwa nguvu na akitakiwa tena aandike
kuwa alikuwa na mpango wa kumdhuru Dk. Slaa kwa kumpa sumu,
Kutokana na uchovu aliokuwa nao aliamua kukiri kufanya hivyo huku akirekodiwa.
Mlinzi
huyo ameenda mbali zaidi na kufichua mipango ya kigaidi
inayofanywa na Chadema huku akisema wameandaa ofisi za kigaidi.
“Chama ambacho kinandoto ya kuchukua nchi leo kinaandaa mipango ya mauaji na utesaji kama walivyonifanyia .
"Waliniteka na kunifungia kwenye chumba cha mateso wanachomiliki wao, wamenichoma visu na kuniweka kwenye Mashine ya umeme bila kosa lolote,eti wakinishinikiza nitaje wanaonituma.” .
"Waliniteka na kunifungia kwenye chumba cha mateso wanachomiliki wao, wamenichoma visu na kuniweka kwenye Mashine ya umeme bila kosa lolote,eti wakinishinikiza nitaje wanaonituma.” .
Aidha, Kagenzi amekitupia lawama chama hicho na kusema kuwa mateso waliyompa yamemfanya apoteze nguvu za kiume .
Mlinzi
huyo amemalizia kwa kusema kuwa hajawahi
kufanya jambo lolote la kutaka kumdhuru Slaa, na hata kiasi cha fedha
kilichotajwa kuingiziwa na watu wa usalama wa taifa si kweli na hawezi
kutunza fedha katika simu.
Ameeleza pia kwamba amefanya mambo mengi kwa
Dk. Slaa na hivyo hawezi kumdhuru licha ya kufahamu siri zake
nyingi.