Simanzi ilitawala katika Hospitali ya Wilaya ya Mafinga wakati maiti zilizopatikana kwenye ajali mbaya iliyotokea mapema leo asubuhi,maeneo ya Changarawe, Mafinga
Mkoani Iringa,zikiwasili.
Zaidi ya watu 40 wamepoteza maisha katika ajali hiyo iliyohusisha Lori la Mizigo na Basi la abiria la Kampuni ya Majinja lililokuwa likitokea Mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar es salaam.
Zaidi ya watu 40 wamepoteza maisha katika ajali hiyo iliyohusisha Lori la Mizigo na Basi la abiria la Kampuni ya Majinja lililokuwa likitokea Mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar es salaam.
Ni majonzi kwa kila alefika kwenye hospitali hii.
Sehemu
ya Wasamaria na Mafundi waliosaidia kazi ya kuyatenganisha magari hayo
wakiangalia kama kuna watu waliosalia kwenye basi lililopata ajali leo
kwa kugongana na kuangukiwa na lori la Mizigo.
Lionekanavyo basi hilo kwa nyuma.
Basi hilo linavyoonekana baada ya ajali hiyo ambayo imeleta majonzi makubwa sana kwa Taifa.
Kontena la Lori hilo likiwa limewekwa pembeni baada ya kuondolewa kwenye eneo la Ajali.