MAPOKEZI YA ZITTO KABWE YAFUNIKA MBAYA KIGOMA KASKAZINI, JIONEE MWENYEWE PICHA

Baada ya kutemwa na CHADEMA, Zitto Kabwe aenda jimboni kwake Kigoma Kaskazini kuzungumza na wananchi wake. 

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe amewataka wakazi wa Kigoma kutosikitishwa na mambo yanayomkabili kwa sasa ila wamuunge mkono kwa hatua yoyote atakayoichukua kwa kuwa ni wanasisasa wengi wamepitia katika misukosuko kama yake.

Zitto ametoa kauli hiyo Kigoma alipokutana na viongozi 250 wa vijiji Kigoma alipokutana nao LEO.

“Msinililie mimi kwa kuwa haya ni mapito ya kila mwanasiasa makini, wengi walitofautiana na vyama vyao kwa sababu ya ya maslahi ya mataifa yao.. hivyo jukumu kubwa ni kuniunga mkono…”

Mbunge huyo amesema hadi sasa hajapewa taarifa yoyote ya kusitishwa kwa Ubunge wake, lolote likitokea atarudi kuwafahamisha juu ya uamuzi wake.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo