Mama mmoja kutoka nchini Nigeria ameweka laana hadharani kwa bintiye ambaye aliolewa bila kumualika.
Mama huyo aliyekuwa na hasira alisema aliteseka kumzaa bintiye kwa jina Chinyere na alibaki ameduwaa kupuuzwa siku ya harusi yake. Kulingana na mwanamke huyo, hakualikwa wala kufahamishwa kuhusu harusi hiyo iliyofanyika katika jimbo la Enugu.
Mama huyo alizungumza kwa uchungu kwenye video iliyochapishwa Twitter na @instablog9ja. Alisimulia jinsi alivyoteseka kujifungua Chinyere na pia kumsomesha.
Mwanamke huyo alisema Chinyere na mumewe watateseka sana maishani kwa kutomwalika au kumjulisha kuhusu mipango yao harusi.
Mom lays cur§£s on her daughter for getting married without informing her
— Instablog9ja (@instablog9ja) February 7, 2023
pic.twitter.com/r3QgsZPDqN