Ajali hiyo ilitokea baada ya basi la
abiria la kampuni ya Majinja Express lililokua likitokea Iringa
likielekea Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na lori lililokua
likitokea Dar es Salaam kuelekea Iringa.
Mkuu wa polisi katika
mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi, amethibisha kutokea kwa ajali hiyo na
kusema kuwa kati ya watu 41 walioaga dunia, wanaume ni 33, wanawake 5 na
watoto watatu.
Taarifa zaidi kutoka kwa watu walio katika eneo hilo zinasema kuwa miili ya maiti 32 bado haijatambuliwa na ndugu ama jamaa.
Mkuu wa polisi katika mkoa wa Iringa, ameelezea chanzo cha ajali hiyo akibaini kwamba dereva wa lori alijaribu kukwepa moja ya shimo katika barabara suala lililomsababisha kutoka katika upande wake wa barabara hadi upande wa basi hilo na kusababisha kugongana na basi hilo la kampuni ya Majinja Express.

Moja wa mashuhuda wa ajali hiyo, Jackson Manga amesema kama dereva wa
basi hilo angezingatia ishara za taa kali alizokuwa akiwashiwa na dereva
wa lori hilo kwa vyovyote vile ajali hiyo isingetokea. Manga amesema
katika eneo hilo lenye mteremko wa wastani, lori lilikuwa likipandisha
na basi lilikuwa likishuka.
Amesema ukaidi wa dereva wa basi ulisababisha dereva wa lori aingie katika shimo kubwa katika eneo hilo hali iliyosababisha ashindwe kulimudu gari hilo kabla ya kuvaana uso kwa uso na basi hilo.
“Baada ya kuvaana, kontena la futi 40 lililokuwa limepakiwa katika loli hilo liliruka juu na kwa kishindo kikubwa, kubamiza na kufunika basi,” alisema.
Mmoja wa majeruhi wa basi hilo, Kevin Humphrey ambaye amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mufindi amesema; “Tulisikia mshindo mkubwa baada ya basi letu kugongana na lori hilo na mshindo huo ulisababisha na kontena iliyotoka kwenye lori hilo na kupiga juu ya basi letu.”

Ajali za barabarani zimekithiri nchini Tanzania. Mwaka 2014 watu zaidi
ya 200 walifariki kutokana na ajali za barabarani. Ajali nyingi
husababishwa na dharau na mwendo wa kasi wa madereva.