skip to main |
skip to sidebar
MAITI ILIYOHARIBIKA VIBAYA YAKUTWA IKILIWA NA PAKA HUKO MOROGORO
Jamaa mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Mbulu amekutwa kwenye
jumba bovu akiwa amekufa kisha mwili wake kutoa harufu kali huku ukiliwa
na paka.
Mwili wa Mbulu ukitolewa ndani ya jumba bovu.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, maiti ya jamaa huyo
iligundulika wikiendi iliyopita katika jumba hilo maeneo ya Mtaa wa Simu
B Kata ya Mji Mpya mkoani hapa ambapo wananchi wa maeneo hayo walisikia
harufu kali kutoka kwenye jumba hilo, walipoingia ndipo wakakuta mwili
wa jamaa huyo huku pua na sehemu za uso zikiwa zimetafunwa na paka.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mwenyekiti wa mtaa huo, Maneno Kifea
’Ticha’ alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.Licha ya harufu kali
mwanahabari wetu alijitosa na kuingia kwenye jumba hilo ambapo
alishuhudia mwili wa jamaa huyo ukiwa umeharibika.
...Mwili ukipakizwa kwenye gari.
Hata hivyo, serikali ya mtaa huo ilitoa taarifa polisi ambao walifika
na kuuchukua kisha kwenda kuuhifadhi kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
wa Morogoro huku uchunguzi ukiendelea juu ya kifo chake.
CREDITS:GPL
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi