Muda mfupi baada ya wakuu wa nchi za Tanzania na Kenya kumaliza mgogoro wa kuzuiwa kwa magari ya Tanzania kupeleka wageni katika uwanja wa ndege wa Jomo nchini Kenya magari hayo leo yameanza rasmi safari zao huku wamiliki wasafiri na madereva wakieleza faraja yao baada ya kumalizika kwa mgogoro huo wa kimaslahi.
blog hii ilifika katika kituo kikuu cha magari hayo jijini Arusha na kushudia magari mengi yakiwa yanaondoka kuelekea Nairobi nchini Kenya ambapo wasafiri kutoka nchi zote mbili wamesema maamuzi hayo ni ya busara kwani walikuwa wanateseka sana kwa kutumia muda mrefu na wengine walilazika kuhairisha safari za kwenda nchi za ulaya na iliwaghalimu.
Kwa upande wao wamiliki wa makapuni yanayotoa huduma hiyo wamesema viongozi wa serikali za nchi hizo wametumia busara kubwa kwakuwa tofauti hizo zimeathiri uchumi wa watu wengi na madereva nao wakidai walikuwa wanapata wakati mgumu katika utendaji wa kazi zao.
Awali akizungumzia sakata ilo waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu aliwataka watanzania wawe na subira wakati serikali inashuhulikia suala ilo ambalo hivi sasa imemalizika kwa amani.