Zaidi ya wanafunzi 200 wa shule ya msingi KINGOLWIRA katika manispaa ya morogoro wamegundulika kuwa na matatizo ya kinywa na meno na baada ya madaktari wa afya ya kinywa katika hospitali ya mkoa wamorogoro kufanya uchunguzi na kuwasafisha meno wanafunzi.
Akizungumza wakati wa zoezi la utoaji wa huduma ya afya ya kinywa na meno katika shule ya msingi KIGOLWIRA na katika kituo cha kulea wazee wasiojiweza cha fungafunga mjini morogoro Daktari wa meno Samson Tarimo amesema baada ya kufanya uchunguzi na kuwasafisha meno wamebaini idadi kubwa ya wanafunzi meno yao yameoza ambapo amewataka wazazi kuwapeleka watoto hospitali kw amatibabu zaidi.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi na wazee waliopata huduma hiyo wameshukuru madaktari ambapo wameeleza walikuwa wakisumbuliwa na tatizo la meno kwa muda mrefu bila kupata ufumbuzina kuiomba serikali kuwezesha juhudi zilizoanzishwa na madaktari hao kuwa endelevu.