East Coast Team imeivaa-King Crazy GK

Rapa King Crazy GK ambae jana ametambulisha wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la 'Shukrani' amefunguka na kusema kuwa wimbo huo ameutoa maalumu kwa ajiri ya kuwashukuru wadau mbalimbali na mashabiki ambao walikuwa wakimsubiri wakati wote



AY/GK/Mwana FA
akiwa masomoni na pia kuwashukuru wasaniii ambao wamepigania kuutangaza na kuufikisha mbali zaidi muziki ukilinganisha na kipindi ambacho wao walikuwa wakifanya muziki.

GK alisema kuwa huu ni kama mwanzo wa mashabulizi hivyo ameona bora kushukuru kwanza kabla ya kazi rasmi kuanza,kwa mujibu wa Gk alisema kuwa baada ya hiii kazi tutegemee kusikia kazi kutoka katika kundi la Muziki wa Hip Hop ambalo lilifanya vizuri miaka ya nyuma East Coast Team ambalo liliundwa na wakali kama Ay,Mwana FA,Buff G,Soud Brouwn,Oten pamoja na amiri jeshi mwenyewe King Crazy GK.

"Wimbo huu nimetoa kwa ajiri ya kuwashukuru wadau wa muziki,mashabiki wangu pamoja na wasanii wenzangu kama kina Vanessa Mdee,Diamond Platnum ambao wameweza kuufikisha muziki mbali zaidi na kupata tuzo mbalimbali nje ya Tanzania,hii inaonyesha wazi kuwa muziki wetu kwa sasa umekuwa hivyo kuna tofauti na miaka ile sisi tunafanya muziki,Mshabiki wategemee kuisikia ile East Coast Team ya zamani maana mpaka sasa kuna kazi tatu zishafanyika na ziko tayari ila tunafanya kuchagua kazi ipi iwe ya kwanza kutoka baada ya hii Shukrani ya kwangu"

Mbali na hili King Crazy GK emeelezea sababu kubwa ya kufanya kazi hii na Vanessa na kusema kuwa aliangalia kwa sasa msanii gani anaweza kusikilizwa na watu wote katika jamiii ndipo alipogundua kuwa Vanessa anaweza kufikisha ujumbe kwa watoto,vijana na hata watu wazima na ndio maana alimua kufanya nae hiyo kazi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo