KATIBU Mkuu
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa
(pichani kushoto) muda huu ametoka katika ofisi za Makao Makuu ya Polisi
jijini Dar es Salaam alipokwenda kupeleka malalamiko yake ya kutaka
kuuawa na mlinzi wake aitwaye Khalid Kangezi.
Dk. Slaa amekabidhi malalamiko yake hayo kwa maandishi ambapo zaidi ya kurasa tisa amezikabidhi kituoni hapo.
Akiongea na
wanahabari, Dk. Slaa amesema kuwa hajaitwa na mtu yeyote kituoni hapo
kuhojiwa kama ilivyodhaniwa hapo awali bali ameenda mwenyewe kwa ajili
ya kukabidhi malalamiko yake.
Dk. Slaa
amekaa ofisini hapo kwa zaidi ya saa tano ambapo waandishi wa habari
walizuiliwa kuingia ndani hivyo kulazimika kusubiri nje ya ofisi hiyo
hadi alipomaliza kuandika malalamiko yake.