Picha za ngono zilizozagaa katika mitandao
ya kijamii za Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’,
zikimuonesha akifanya ufuska na mrembo chumbani zimemliza mchumba’ke,
Siwema ambaye ameamua kumsusia mtoto wao mchanga.
Habari kutoka chanzo cha kuaminika zilisema kwamba, baada ya kusambaa kwa picha hizo kuliibuka tafrani nyumbani kwa wapenzi hao, Kimara jijini Dar ambapo Siwema alidai kuondoka usiku wa manane akimwacha mtoto mchanga.
Baada
ya picha hizo kusambaa, mwandishi alimtafuta Nay ili kuzungumzia
sakata hilo ambapo alikiri kuzijua picha hizo kwamba ni kweli mama mtoto wake huyo
alilia japokuwa alitumia nguvu kubwa kumweka sawa na sasa maisha
yanaendelea.