KUKAMILIKA KWA UJENZI WA ZAHANATI YA NDULAMO MAKETE WANANCHI KUCHEKELEA

Kukamilika kwa ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Ndulamo wilayani Makete mkoani Njombe, kutakuwa ni mkombozi kwa wananchi wa kijiji hicho na maeneo ya jirani kujipatia huduma za afya kwa ukaribu

Hiyo inafuatia jitihada za wananchi wa kijiji hicho kuwa na moyo wa kushiriki kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofika kijijini hapo, ambapo wamesema itawapunguzia kwenda umbali mrefu kufuata huduma za afya

Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Bw Majuto Mbwilo amezungumza nasi kuhusu ujenzi wa zahanati hiyo huku akisisitiza siri ya wananchi hao kuwa na moyo wa kuchangia miradi ya maendeleo ni kuwasomea mapato na matumizi ya fedha walizochanga

Bi Anifa ambaye ni muhudumu wa afya ya msingi kijijini hapo amesema anafuraha kuona zahanati hiyo inaendelea na anaimani itakamilika kwa wakati ili ianze kutoa huduma za afya kwa wananchi hasa kina mama wajawazito waliokuwa wakifuata huduma kwenye hospitali ya wilaya ambayo ipo mbali na kijiji hicho


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo