Ripoti zinazoibuka zimethibitisha kwamba mganga mmoja alikata roho wakati akifanya mapenzi na mke wa pasta katika hoteli moja eneo la Ikere, jimbo la Ekiti.
Jarida la The Punch liliripoti kuwa tukio hilo lilitendeka siku ya Jumatatu, Januari 2 wakati mke wa pasta na mganga walipokutana.
Mmoja wa wakaaji katika eneo hilo ambaye hakutaka atambulike alithibitisha kuwa, mwanamke huyo alikuwa ameolewa na pasta. “Mwanamume huyo aliaga dunia ndani ya chumba cha hoteli wakati akila uroda na mwanamke huyo. Kisha mwanamke huyo akapiga mayowe baada ya kugundua lofa huyo alikuwa amezirai," mkaaji huyo alisema.
Kulingana na aliyeshuhudia kisa hicho, meneja wa hoteli hiyo na baadhi ya wakaaji walikimbilia eneo la tukio na kumpeleka mganga huyo katika hospitali ya karibu, ila alikuwa amefariki. Akizungumzia tukio hilo, msemaji wa polisi Ekiti, Sunday Abutu alisema wananguza kisa hicho. Alifichua kwamba kifo cha mganga huyo kilithibitishwa na kamanda wa polisi wa jimbo la Ekiti, siku ya Jumatatu, Januari 2.
“Tumethibitisha kufariki kwa mwanamume ndani ya hoteli moja eneo la Ikere Ekiti siku ya Jumatatu. Maiti yake imechukuliwa na kupelekwa katika makafani,"msemaji huyo wa polisi alisema. Aliongeza kusema kwamba wanamhoji mwanamke huyo huku wakiendeleza uchunguzi kufichua chanzo cha kifo chake.
Chanzo: TUKO.co.ke