MAMLAKA YA UDHIBITI WA HUDUMA ZA NISHATI NA MAJI (EWURA).
Kuna taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, kuelezea kwamba kutakuwa na mgomo wa wafanya biashara wa mafuta nchini, na kwa hiyo kutakuwa na uhaba wa mafuta ya jamii ya petroli.
Aidha, taarifa hizo zinawachochea watumiaji wa bidhaa hizo kununua kwa wingi ili kuepuka usumbufu.
EWURA inapenda kuutaarifu umma kwamba taarifa hizo si za kweli, hakuna mgomo wala tatizo lolote linaloweza kuhatarisha upatikanaji wa mafuta nchini, na kwamba nchi ina akiba ya kutosha ya mafuta, na hakuna haja ya wadau kuwa na wasi wasi.
Umma unakumbushwa pia kuzipuuza taarifa za namna hiyo kwa sababu ni za upotoshaji na zinalenga kuvuruga hali ya utulivu wa soko la mafuta nchini. Ikumbukwe pia kwamba ni EWURA tu yenye mamlaka ya kisheria ya kuutaarifu umma juu ya hali ya soko la mafuta na upatikanaji wa bidhaa zake.
Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano na Uhusiano, EWURA.