Mkurugenzi wa Kampuni ya Ibraline ,Ibrahim Shayo. |
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Moshi.
SIKU chache baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kutangaza punguzo la bei ya Mafuta Kampuni ya kutoa huduma ya usafirishaji wa ndani na nje ya nchi ya Ibraline imetangaza kushusha nauli kwa nusu ya bei elekezi ya SUMATRA.
Hatua hiyo inakuja wakati baadhi ya wananchi kulalamika kutokuwepo na ahueni yoyote licha ya kwamba serikali imetangaza kushusha bei ya bidhaa ya Mafuta kwa nchi nzima kufuatia bidhaa hiyo kushuka bei katika soko la dunia.
Akizungumza ofisini kwake mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ibrahimu Shayo alisema Kampuni imefikia hatua hiyo ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa wateja wake ambao wamekuwa wakitumia huduma ya usafiri inayotolewa na Ibraline.
“Tumeamua kufanya hivi lengo ni kuwashukuru wateja wetu wanao tumia huduma ya usafiri unaotolewa na kampuni yetu ya Ibraline…ningewajua mmoja mmoja ningeweza kuwapa mkono lakini kwa kuwa wanaishi maeneo tofauti ndio sababu tumeamua kurudisha kile tunachopata kwa njia ya kuwapunguzia bei.”alisema Shayo.
“Hivyo basi kuanzia sasa magari yetu yatatoa huduma zake kwa nusu ya bei elekezi inayotolewa na Mamlaka ya Udhibiti, Usafiri wa nchi Kavuna Majini (SUMATRA) ambapo abiria watatozwa kiasi cha Shilingi 17,000 badala ya 33,300 kwa usafiri wa kwenda na kutoka Dar es Salaam wakitokea Arusha.”aliongeza Shayo.
Alisema unafuu wa ofa hiyo abiria wataipata endapo watafika moja kwa moja katika ofisi za kampuni hiyo zilizoko Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Dar es Salaam badala ya kutumia mawakala wanaopatikana katika vituo vikuu vya mabasi katika mikoa hiyo.
“Unafuu wa gharama ya nauli utaipata pekee endapo utafika ofisi za kampuni yetu zilizoko mikoani ambapo kwa Arusha ofisi ziko Kibla,Kilimanjaro tunapatikana barabara ya Ghala jirani na kiwanda cha kubangulia Kahawa (Cofee Curing) na Dar es Salaam tuko Ubungo ofisi namba 19.”alisema Shayo.
Aidha Shayo alisema hivi sasa Kampuni yake imeanzisha safari za kuelekea Masasi mkoani Mtwara baada ya kupokea maombi ya wakazi wa maeneo hayo na kampuni kuamua kutoa gari tatu za kisasa kwa ajili usafiri wa kuelekea huko.
Alisema kampuni ya Ibraline inategemea kuanza kutoa huduma ya usafiri kwa mikoa zaidi ya nane na kwamba kinachofanyioka sasa ni kuangalia uwezekano wa namna gani inaweza kuingia mikoa ya Dodoma ,Morogoro na
Mbeya.
Juzi baadhi ya wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro walidai hakuna haueni yoyote wanayopata licha ya kushuka kwa huduma hiyo.
Baadhi ya wakazi hao ,Joachim Kimaro, Andrea Lyimo na Yusta Mafangavo waliliambia globu ya Jamii kuwa wanaofaidika na kushuka kwa bidhaa za Mafuta zaidi ni wamiliki wa vyombo vya usafiri .
“Wamiliki wa magari ya biashara kama mabasi na magari makubwa ya kusafirisha mizigo ndio wamenufaika na kushuka kwa bei ya mafuta ,kwa sababu nauli za kusafiria hata kusafirisha mizigo hazijashuka bado ziko pale pale.”alisema Kimaro.
Alisema wengine wanao nufaika na kushuka kwa bei ya mafuta ni wafanyabiashara wa bidhaa katika maduka ambao licha ya kununua mafuta ya taa kwa bei elekezi ya EWURA bado wameendelea kuuza bidhaa hiyo kwa mtumiaji wa kawaida kwa bei ile ile ya zamani.