Wema Sepetu Hajampeleka Diamond Mahakamani Kwa Deni La Milion 10 – Martin Kadinda


Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda amekanusha taarifa zilizoandikwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini likiwemo gazeti la Mtanzania kuwa amempeleka Diamond polisi kwa kile kinachosemwa ni kumtapeli shilingi milioni 10.
 
Martin amesema kuwa Wema na Diamond hawadaiani chochote na kwamba habari hizo ni za uongo.
 
“Unajua tatizo ni kwamba hatujajua source ni nani. Kwa sababu taarifa ikishaingia kwenye social network everybody posts, kwahiyo sisi tunamtafuta nani ameianzisha hiyo stori.
“We don’t have any issue with Diamond. Diamond hana issue yoyote na Wema,” amesisitiza.
 
“Kwahiyo tunashangaa ni kama ambavyo wanazusha sijui kafumwa na nani ni uongo mtupu. Lakini nashangaa media ambazo zinaaminika zinaamua kuandika story bila kumpigia simu mhusika au meneja na kuuliza ukweli wa hiyo story.”


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo