Wanafunzi wakosa Makazi baada ya Mabweni kuungua moto


Wanafunzi 64 wa kike wanaosoma kidato cha tano na cha sita katika shule ya sekondari ya Mpwapwa iliyopo mkoani Dodoma wamehifadhiwa katika mabweni ya chuo cha ualimu Mpwapwa kufuatia bweni lao kuteketea kwa moto juzi.

Akithibitisha kutokea kwa moto huo mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Christopher Kangoye alisema kuwa wamelazimika kuwahamishia wasichana hao katika mabweni ya chuo cha ualimu Mpwapwa kutokana na moto huo kuteketeza kila kitu kilichokuwemo ndani ya bweni lao.
 
Mkuu wa shule hiyo Nelson Milanzi amesema kuwa moto huo ulianza majira ya saa 3:20 jana asubuhi wakati wanafunzi hao wakiwa madarasani ambapo moto huo uliteketeza kila kitu kilichokuwemo bwenini na kuwaacha wanafunzi hao wakiwa hawana mahali pa kulala wala nguo za kubadilisha.
 
Hata hivyo chanzo cha moto huo bado hakijajulikana ambapo kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma amesema kuwa jeshi hilo linashirikiana na shirika la umeme wilayani humo ili kujua chanzo cha moto huo, na hakuna taarifa za kifo zilizoripotiwa katika tukio hilo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo