Kwa mujibu wa gazeti la mtanzania Mbunge wa Musoma vijijini Nimrod Mkono wa CCM amenusurika kutekwa na
watu wasiojulikana katika eneo la Tanki bovu jijini Dar es salaam.
“Nikiwa na msaidizi wangu tukitoka Bagamoyo tukiwa ndani ya gari
langu aina ya Marcerdez Benz katika eneo la Tank bovu gafla yalitokea
magari mawili na kutuziba kwa mbele lakini dereva baada ya kuona hali
iyo aliondoa gari kwa kasi akipita pembeni na kufainikiwa kutoka eneo
hilo”alisema Mkono.
Alisema baada ya kutoka eneo hilo magari hayo aligeuza na kumfuata
yakiwa mwendo kasi na baada ya kuwafikia kijana mmoja aliyekua amevaa
miwani nyeusi alishusha kioo na kututaka tusimamishe gari.
“Dereva wangu aliondoa tena gari kwa kasi hadi njia panda ya Kawe
ambapo tulimkuta askari wa zamu na kumwelezea na kuomba msaada wake na
baada ya muda kidogo magari hayo yaliwapita kwa kasi eneo hilo
yakielekea Mbezi Beach na askari yule alitushauri kwenda kutoa taarifa
kituo cha polisi”alisema.
